Mwanablogu aliyetusi uislamu kuadhibiwa
Mahakamu kuu nchini Saudia imeamua kuwa hukumu ya kifungo cha miaka 10
na viboko 1000 dhidi ya mwanablogu Raif Badawi aliyepatikana na hatia ya
kutukana Uislamu itabaki kama ilivyo.
Utalawa nchini Saudi Arabia
uliamuru kusikilizwa tena kwa hukumu hiyo kufuatia shutuma za kimataifa
baada ya Badawi kuchapwa viboko hamsini mapema mwaka huu.Mkewe na makundi ya haki za kibinadamu yameonya kuwa huenda akafariki ikiwa hukumu hiyo yote itatekelezwa.
Badawi alikamatwa kufuatia blogi aliyoanzisha ambayo ilikashifu baadhi ya tamaduni nchini Saudi Arabia.
No comments:
Post a Comment