Marekani imerudi tena kwenye Headlines za ubaguzi.. hii imetokea ndani ya ndege ikihusisha soda ya kopo !!
Neno
ubaguzi ni kama lilianza kusahaulika hivi duniani.. lakini kwa sasa
linasikika karibu kila siku, matukio ya watu wenye asili ya Afrika
kupigwa risasi Marekani yalichukua headlines kubwa sana na bado
hayajasahaulika !!
Hiki kilichofanywa na mhudumu wa kwenye ndege ya Shirika la ndege la United Airlines, nacho kimelalamikiwa na kuhusishwa na ishu ya ubaguzi.. mhudumu huyo aligoma kumpatia abiria mmoja mwanamke, Tahera Ahmed soda ya kopo, alichomjibu ni kwamba eti hawezi kumpa kwa sababu anaweza kutumia kopo hilo la soda kama silaha ndani ya ndege.
Kitu kilichomkasirisha zaidi Tahera ni
ishu ya yeye kukataliwa soda ya kopo alafu jirani yake akapewa bia ya
kopo.. mwanamke huyo akalalamika kwamba labda kwa vile yeye ana asili ya
Kiarabu ndio maana akakataliwa !!
Kwa habari, matukio na michezo moto moto, ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment