Alitamani kuwa na makalio makubwa, baada ya kujichoma sindano matokeo ilikuwa ni stori nyingine !!
Ishu ya wasichana na wanawake kupenda
kuongeza maumbile ya miili yao limekua kama ishu ambayo imechukua sana
nafasi sehemu mbalimbali duniani.
Tunashuhudia watu wengi wakiongeza
makalio kwa kusudi la kuwa wenye mvuto zaidi, na kumekuwepo na vidonge
na sasa kuna sindano za kuongeza makalio.
Leo nimekutana na stori iliyotokea Los Angeles Marekani, ambako msichana Kelly Mayhew mwenye miaka 34 amefariki baada ya kufikishwa St.John’s Espiscopal Hospital, muda mfupi baada ya kuchomwa sindano ya kuongeza makalio.
Kelly Mayhew na mama yake walisafiri kutoka Maryland kwenda Rockaway, walikokua wameelekezwa na rafiki yake Kelly
ili kwenda kuchoma sindano hiyo ambayo ilikua inatolewa kinyume na
utaratibu… mtoaji wa huduma hiyo alijiita daktari lakini hakuwa
amesajiliwa na alikuwa hatambuliki kisheria.
Baada ya kuchomwa sindano hiyo Kelly alianza kupumua kwa shida, akawa anajitupa ovyo chini huku akiishiwa pumzi… baada ya kuhangaika kwa kama dakika ishirini hivi, Kelly alifariki akiwa kwenye mikono ya mama yake.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment