BRAZIL
imemfukuza kazi kocha Carlos Dunga baada ya matokeo mabaya kwenye
michuano ya Copa America Centenario inayoendelea nchini Marekani.
The
Selecao wametolewa kwenye hatua ya makundi tu ya mashindano hayo baada
ya kutoa sare na Ecuador na kufungwa na Peru, licha ya kushinda 7-1
dhidi ya Haiti.
Nafasi
yake inatarajiwa kuchukuliwa na kocha wa Corinthians, Tite, ambaye
ataiongoza timu hiyo katika michuano ijayo ya Olimpiki nchini Brazil.
Dunga
aliingia kwenye mashindano hayo akiwa katika wakati mgumu baada ya timu
kucheza vibaya kwenye mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2018 na pamoja na
matokeo mabaya ya Marekani, imesababisha kufukuzwa kwake.
Kocha
Carlos Dunga amefukuzwa kazi Brazil baada ya matokeo mabaya kwenye
michuano ya Copa America Centenario inayoendelea nchini Marekani
No comments:
Post a Comment