Wednesday, June 15, 2016

KABURI LA MTU WA AJABU TANGA LAGUNDULIWA, ALIKUWA NA SAUTI ISIKIKAYO ZAIDI YA KLM 5


Tangakumekuchablog
Tanga, Kwa mujibu wa Wikipedia, Robert Pershing Wadlow, ambaye ameishi kati ya February 22, 1918 na July 15, 1940, ambaye pia alijulikana kama Jitu la Alton na jitu kubwa la Illinois, alikuwa ndiye mtu mrefu aliyewahi kuwekwa katika kumbukumbu za Kitabu cha kumbukumbu za Guiness.
Urefu wa Wadlow ulifika futi 8 na inchi 11.1 au sentimita 2.72 na alikuwa na uzito wa pauni 439 au kilo199 wakati wa kifo chake akiwa naumri wa miaka 22.
Kisayansi umbile lake kubwa kuendelea kukua kwake wakati wa utu uzima umetokana kuwepo kwaukuajiusio wa kawaida unaotokana na kuongezeka kwa seli katika kiungo kiitwacho pituitary gland,kitu ambacho kinasabaisha kuwepo kwa kiasi kikubwa cha homoni za ukuaji. Hakuonesha kuacha kukua hata wakati a kifo chake
Mtu huyo alikuwa na urefu wa futi tatu alipokuwa mtoto anliweza kumbeba baba yake alipokuwa na umri wa miaka tisa. Mikono ya Wadlow iliweza kufikia futi tisa na inchi tano ikipanuliwa na viganja vyake violikuwa na ukubwa wa futi moja.
Wadlow's alipofariki jeneza lake likuwa na uzito wa pauni 1,000 na lilihitaji wabebaji 18 ambao walilibeba  kulifikisha mahali pake pa mapumziko ya mwisho Alton, Illinois. Familia ya Wadlow iliamua kuharibu vitu vyake kwa hofu kuwa vinaweza kukusanywa na kuenyesha katika maionyesha kana vitu vya ajabu vya kumbukumbu
Hata hivyo, utafiti wa miaka 16 uliofanyika huko Handeni unaonyesha kuwa Tanzania inaweza kuwa na historia ya mtu mrefu zaidi duniani.
Katika hali ya kawaid si rahisi kuamini kuwa kuna mtu mwenye urefu wa futi 35, lakini utafiti wa hivi karibuni umegundua kitu ambacho kimeelezwa kuwa ni ajabu sana juu ya maajabu hayo
Huko katika cha Ngwujini, wilayani Handeni mtafiti mmoja wa mambo ya kale na ya asili, Ramadhani Ayubu amegundua kitu cha ajabu. Mtafiti huyo ambaye amefanya kazi yake hiyo kwa miaka 16 amgundua kaburi lamtu mmoja wa ajabu ajulikanaye kwa jina la Mbulushi Malilo.

Mtu huyo ambaye kaburi lake lilipimwa na kufikia futi 35 anaelezwa kuwa mtu waajabu sana alieyishi katika karne ya 16 ambaye alikuwa na nguvu za ajabu. Kwa mujibu wa Mtafitia Aybu mtu anasemekana kuwa aliwahi kuchiimba bwawa ambalo hadi sasa linatumika na alikuwa na sauti kubwa ambapo hata akiita mtu inasikika kwa kilomita moja.

Kwa mujibu wa Ayubu, ambaye anamiliki kampuni inayoitwa Regulate Body Temperature Cilini iliyoko Amana, jijini Dar es Salaam mtu huyo anaidaiwa kuwa alikuwa mtaalamu wa masuala ya kivita na alitumika hata hata katika vita mabvyo watu mashuhuri kama OleTiptip na Bushiri walipigana na watawala.

 Ayubu, ambaye anadai kuwa alisoma Ethiopia masomo ya Sayansi na akalazimika kuacha kutokana na mgogoro wa mpaka kati ya Ethiopia na Eritres alidai kuwa kabla hajafa aliweka wosia kuwa lazima akifa azikwe Ngugwini.

Akielezea namna alvyofahamu juu ya hadithi za mtu huyo, mtafiti huyo wa mambo ya mazingira na mambo ya kale, alisema kuwa alipata kujua habari zamtu mtu kutoka kwa watu wa familia ya Mbulushi ambao alikutana nao Same, mkoani Kilimanjaro. Alielezwa kuwa katika kaburi lake alikuwa amezikwa na mkuki wake.

Ndipo nilipoamua kwenda huko Ngwujini lakini nilipopata taabu sana kwa sababu wanakijiji walikuwa wanaona ajabu mimi kufuatilia kaburi ambalo walikuwa wanaliona kama kaburi la kawaida sana, alisema Ayubu ambaye alisema kuwa imechukua miaka 16 kwa wanakijiji hao kukubali kuwa kaburi ni la mtu wa ajabu sana.

Alisema kuwa vijana, wazee na wanawake baada ya ugunduzi huo walikuwa hawaamini na wanauliza kwa nini kaburi, kama ni la mtu wa ajabu halijulikani. Wanasema kuwa hawaoni kuwa kuna faida yoyote kwa kuwepo kwa kaburi hilo.

Eneo hilo lenye kaburi linafanywa na wakazi wa eneo kamaeneo la mizimu na kuna mti wa aina ya mkuyu ambao watu wanaamini hata ukikatwa utaendelea kusimama hivyo hivyo. Eneo hilo wanakijiji wameamua kulihifadhi lakini linakabiliwa na tishio la kukatwa kwa miti.

Kwa mujibu wa amtu mmoja aitwaye Omari Athumani, almaarufu kwa jina la Mganga ambaye ni wa kizazi cha Mbulushi ambao wanatunza kaburi hilo, hapo mwanzoni  kulikuwa na msitu mkubwa. “Miti ilikuwa inavuma sana lakini hakuna miti. Msitu umekatwa,” alisema

Aliendelea kusema kuwa historia na utamaduni sasa hivi vimepotea na kudai kuwa kulikuwa na nyani ambaye akipita tu mvua inanyesha lakini sasa hivi amepotea kutokana na msitu kukatwa.

Mganga pia alieleza kuwa kwenye bwawa ambalo anadai limechiimbwa na Mbulushi peke yake kuna mamba ambaye hatoki mpaka aitwe.

Naye Sudi Mohamed Mgweno amefafanua zaid kuhusu mti ambao wanaamini ukikatwa unaendelea kusimama, alisema kuna mwaka watu kutoka Kenya walikuja kukata miti kwa ajili ya mbao na walikata mti huo. Amesema kuwa walikata mti huo kwa sababu ulikuwa unavutia kutokana na ukubwa wake. “Mti huo ulikatwa na kusimama tena,”alisema.

Nao vijana mmoja Swedi Ramadhani na Juma Said walisema kuwa wanaamini kuwepo kwa kaburi hilo kunaweza kuleta fursa za maendeleo ambazo hazikuwepo hapo awali pamoja na kuwepo kwa raslimali hiyo ya watu wa kale.

                                                                  Mwisho
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mvumbuzi Ramadhan Ayoub simu 0717 720221
 
 Wakazi wa kijiji cha Ngugwini Kabuku Wilaya ya Handeni Tanga wakilifanyia usafi Kaburi la Mbulushi ambaye alikuwa mtu wa ajabu ambapo watawala wengi walipata mbinu za kivita kutoka kwake.




No comments:

Post a Comment