Rais Obama alaani mauaji ya Orlando

Polisi nchini humo wamesema kuwa ni shambulio baya kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo.
Rais Obama amesema Marekani inaungana ikiwa na huzuni,mshtuko mkubwa na inalenga kutetea watu wake, pia amesema mauaji hayo yanawakumbusha ni namna gani ilivyo rahisi kupata silaha hatari nchini Marekani.
Shirika la kijasusi nchini humo,FBI limemtambua mshambuliaji huyo kuwa raia wa Marekani,Omar Mateen ambaye naye aliuawa wakati wa mapambano na vikosi vya usalama katika klabu hiyo ambayo ilikuwa na zaidi ya watu 300 ndani yake.
No comments:
Post a Comment