Saturday, June 11, 2016

UJEZI WA NYUMBA ZA WAHANGA WA TUKIO LA MAUAJI KIBATINI WAENDELEA KIOMONI



Ujenzi wa nyumba za muda kwa familia za wahanga wa tukio la mauaji ya watu nane kuchinjwa kijiji cha Kibatini kata ya Mzizima Amboni Tanga na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi ukiendelea kijiji cha Kona Zedi kata ya Kiomoni Tanga.







 Mhanga wa tukio la mauaji kijiji cha Kibatini kata ya Mzizima Amboni Tanga, Mrahagwa Magwe (75) akiwa uwanjani kijiji cha Kona Zedi kata ya Kiomoni Tanga  alikokimbilia baada ya kuyahama makazi yao, Mzee huyo kwa sasa analala nje usiku mchana mvua jua na kutojua hatma yake na vifaa vyake vya ndani.
Kwa sasa mzee huyo wa makamo anaishi uwanjani kulinda thamani zake ikiwemo vitanda na magodoro ambayo nyakati za mvua zimekuwa zikinyeshewa na mvua. Mzee huyo analalamika nyakati za usiku kupigwa na baridi kali hivyo kuwaomba wasamaria wema kumsaidia kwa lolote ili kuweza kujisitiri. 
Mzee huyo amekuwa akishinda katika vyombo vyake ili kuepuka kuibiwa au kuharibika na wapita njia.




Kwa habari, matukio na michezo ni  hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment