Vilevi uwanjani marufuku EURO

Waziri wa mambo ya
ndani nchini Ufaransa, Bernard Cazeneuve,amewataka waandaaji wa michuano
ya bara la ulaya ya Euro 2016 juu ya kukataza vilevi katika maeneo ya
michezo.
Amesema maeneo ya michezo ni nyeti wakati mechi
zikichezwa na hata siku moja kabla ya michuano. Tamko hilo limekuja siku
tatu baada ya fujo kuibuka kutoka kwa mashabiki wa Marseille ambao
walikua wamelewa. Shirikisho la soka barani ulaya,UEFA wameionya England
na Urusi kuwa ziko kwenye wasiwasi wa kutolewa katika mashindano ya
michuano ya soka barani ulaya mwaka huu,euro 2016 kama mashabiki wao
wataendelea kufanya fujo. Michuano hiyo ya UEFA imeomba radhi kwa hali
ya utovu wa nidhamu au vurugu zilizojitokeza kati ya urusi na mashabiki
wa waingereza huko MarseilleBBC
No comments:
Post a Comment