Tangakumekuchablog
Tanga, IMAMU
Mkuu wa Msikiti wa Ibadhi Tanga, Sheikh Mohammed Said, amewataka Waumini wa
dini ya Kiislamu wenye uwezo kuwasaidia masikini ili kuweza kutekeleza ibada ya
funga kama wenzao.
Akihutubia katika swala ya Ijumaa juzi
ikiwa ni ya mwanzo ndani ya mfungo wa mwezi Mtukufu wa Rmadhani, Mohammed
alisema kuna waumini wengi wanafunga lakini hawajui cha kufutaria muda wa
jioni.
Alisema mwezi mtukufu wa Ramadhani
ni mwezi wa kufanya Ibadan a kutoa ili kuweza kupata rehema na msamaha kwa
Mwenyezi Mungu hivyo kuwataka kuisaidia jamii hiyo ili kuweza kuitekeleza Ibada
hiyo.
“Ndugu zangu Waislam tuko katika
kumi la kwanza la mwezi mtukufu wa ramadhani, ni mwezi wa kheri na machumo kwa
mwenye kuzingatia sambamba na mwezi wa toba” alisema Sheikh Mohammed na
kuongeza
“Mwezi huu huja mara moja kwa mwaka
hivyo inatupasa kuuzingatia na kufanya kila ambalo tunaamini kuwa ni jema na
kuweza kuifikia daraja ya mcha Mungu kama wenzetu walivyotutangulia” alisema
Aliwataka watu hao wenye uwezo
kuhakikisha waumini wenzao ambao hawana uwezo kuwasaidia kwa hali na mali ili
funga yao isiwe ngumu bali kuwa na wepesi na furaha wakati wa kufuturu.
Akizungimzia kuhusu wafanyabiashara
kufanya uadilifu na kuuza vyakula kwa bei ya biashara, alisema mwezi huu sio wa
kujitafutia utajiri hivyo kuwaasa kuacha kuwalangua wafungaji.
Alisema vipindi vya mwezi wa
Ramadhani baadhi ya wafanyabiashara
wamekuwa wakiongeza bei za vyakula ambavyo hutumika kwa futari jambo
ambalo ni makosa na huondosha baraka ya biashara.
“Niwakumbushe wafanyabiashara kuacha
kupandisha bei za vyakula kwani kufanya hivyo kutawafanya wafungaji kumudu
gharama za maisha hasa kuipindi hiki cha mfungo” alisema Mohammed
Aliwataka waumini wa dini hiyo
kuwafanyiana wema pamoja kuhurumiana
kwani na kuutaja mwezi huo ni wa baraka wenye ujira mkubwa kwa kila
jambo ambalo mtu hufanya.
Mwisho
No comments:
Post a Comment