Tuesday, March 31, 2015

MTOTO WA MIAKA MIWILI AVUNJA RECORD YA KULENGA SHABAHA

Hii ndio rekodi iliyovunjwa na mtoto wa miaka miwili India

dolly-archer_650x400_81427214935Mara nyingi wazazi hushauriwa kuona umuhimu wa kukuza vipaji vya watoto wao tangu wakiwa wadogo, taarifa ikufikie kuwa mtoto mwenye umri wa miaka miwili ameweka rekodi nchini India kutokana na uwezo wake wa kulenga shabaha ya mishale.
_81884282_81884281Kutokana na vitabu vya kumbukumbu vya rekodi za taifa hilo, mtoto huyo Dolly Shivani Cherukuri, ameweka rekodi ya kuwa mshiriki mwenye umri mdogo zaidi kupata alama 200, katika mashindano yaliyofanyika wiki iliyopita.
288889-2681ba7e-d234-11e4-a4a5-09d7e9cc7466Jarida la Press Trust la India, limesema mtoto huyo alirusha mishale 36 kutoka umbali wa mita 5 na mita 7 na kupata alama 388, tukio lililoshuhudiwa na wachezaji wakongwe na maafisa kutoka idara ya kumbukumbu za michezo.
dolly-archer_650x400_81427214935Baba yake Cherukuri Satyanarayana ambae ni mmiliki wa club moja inayofundisha kurusha mishale amesema, alimfundisha kurusha mishale tangu alipozaliwa, kwa sasa ana mpango wa kumpeleka kushiriki katika mashindano ili afikie hatua ya kuingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness.
290181-0a8223fe-d234-11e4-a4a5-09d7e9cc7466


Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

MAJIJI 10 YENYE FOLENI KUBWA DUNIANI

Sahau kuhusu Dar!! CNN wanasema haya ni majiji 10 yenye foleni kubwa ya magari duniani

trafficNajua Dar es salaam ipo kwenye hesabu ya majiji yenye foleni Afrika Mashariki lakini fahamu tu Dar haipo kwenye list ya majiji yenye foleni kubwa sana wakati wa jioni duniani.
Pamoja na kwamba Dar es salaam inaweza kukuchelewesha kwenye foleni kwa zaidi ya mpaka dakika 60 kufikia saa kadhaa kulingana na umbali wa safari yako, hesabu hii ya utafiti inaonyesha pia baadhi ya miji ambayo inaucheleweshaji mdogo kuliko Dar na baadhi ya comments za watu zimekua za ukosoaji wa ripoti yenyewe kwamba haiko sawa.
a1
Istanbul Uturuki ndio wamechukua nafasi ya kwanza.
a2
Moscow Urusi wamechukua nafasi ya pili
a3
Saint Petersburg ni mji mwingine wa Russia kwenye hii list, unaambiwa kwa mwaka hawa jamaa hupoteza saa 110 kwenye foleni.
a4
Mexico City Mexico wamechukua namba nne ambapo wanasema foleni yake huifanya safari kuwa kati ya dakika 30 mpaka 58.
a5
Wachina na mji wao wa Chongqing ndio namba five kwenye hii list
a6
Recife Brazil ndio namba 6.
Bucharest Romania ndio namba 7 kwenye hii list,
Bucharest Romania ndio namba 7 kwenye hii list,
a8
Namba 8 ni Rio de Janeiro unakua mji wa pili kutoka Brazil kuingia kwenye hii list.
a9
Namba 9 ni Shenzhen ni mji mwingine wa China kwenye list hii, wanasema Madereva hutumia mpaka dakika 24 kwa safari moja.
a10
Namba 10 ni Los Angeles Marekani.

MAMBO YA MAY 1 HAYOO

Kwenye siku ya Wajinga leo, Nay wa Mitego kasema anamuoa huyu

Nay 1Nimeamua kuoa kabisaa.. Kesho(Leo) nitakua nafunga ndoa, huyu ndo mke wangu… Apa sasa ata nikifumania nitapigana mpaka mwisho, na nitakua na haki ubachela byeee Kule sirudi tenaaaaa, Kwa niliowaalika karibuni I hope mtaenjoy‘ ndio kaandika hivyo Nay wa Mitego
Nay 2
Nay 23

MUHAMMADU BUKHARI AIBUKA KIDEDEA NIGERIA

Matokeo rasmi ya Uchaguzi Mkuu Nigeria yanaonesha Wanigeria wameamua hivi..

Muhammadu-Buhari-speech
Siku ya MARCH 28 2015 itakuwa kwenye historia za matukio ya kukumbukwa zaidi Nigeria, walikuwa wakifanya Uchaguzi Mkuu ambapo macho ya wengi Afrika yalikuwa kwenye uchaguzi huo.. Ushindani ulikuwa mkubwa kati ya Rais Goodluck Jonathan ambaye alikuwa madarakani na Muhammadu Buhari.
Kiongozi wa wa chama cha upinzani cha Nigeria ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Muhammadu Buhari amemshinda Goodluck Jonathan kwa zaidi ya kura Mil.2.5.
Goodluck Jonathan alimpigia simu Jenerali Buhari kumpongeza kwa ushindi huo wa kihistoria, ambapo Buhari anakuwa Rais wa kwanza kuongoza nchi hiyo akishinda kutoka Chama cha upinzani.
150120133956_buhari_kano_640x360_ap_nocredit
Nigeria ni moja ya nchi za Afrika ambazo ziliwahi kukumbwa na misukosuko ya Mapinduzi ya Kijeshi, Jonathan amesema katimiza ahadi yake kwamba Uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki; “I promised the country free and fair elections. I have kept my word“– Rais Goodluck Jonathan.
Buhari ni mmoja ya wanasiasa ambao waliungwa mkono na mastaa wakubwa wa muziki Nigeria, Tiwa Savage na kundi la Mavins ni sehemu ya waliomsapoti.

AMKA NA MAGAZETI NA KUMEKUCHABLOG

Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kwa kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita kwa wale wanaorisiti. Kituo pia kinatoa kozi ya Kiingereza na Computer. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB. Simu 0715 772746

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.Kwa matukio na habari za papo hapo usiache kuperuz www.tangakumekucha.blogspot.com

ABDUL BONGE AZIKWA KWAO

Kesi ya AT imeisha? Izzo B na show yake Mbeya na mazishi ya Abdul Bonge.

Rock concertIle kesi iliyokuwa imefunguliwa na mganga aliyedai kuwa anamdai msanii AT imemalizika rasmi jana baada ya kukata rufaa, AT amesema kesi hiyo imemalizika rasmi jana baada ya mganga huyo kukata rufaa lakini alikosa ushahidi na baadae iligundulika kuwa hakuwa na sifa za kuwa mganga  kwa kuwa alikuwa hajasajiliwa kufanya kazi za uganga.
izzoWeekend hii msanii Izzo Bizness atafanya show Mkoani Mbeya ambayo imepewa jina la ‘Home Sweet Home Easter Season Concert‘, Izzo amesema show hiyo itafanyika tarehe 05 April, safari hii itakuwa tofauti kwa kuwa anategemea kuambatana na producer Duppy kwa ajili ya kufanya usaili na mtu atakaeshinda atafanyanae kazi, pamoja na surpise nyingi ikiwemo kuonyesha live video ya wimbo wake wa ‘Kidawa’ kwa mara ya kwanza.
MSIBAWAABDULBONGE5Leo wasanii mbalimbali pamoja na wadau wa muziki wamekutana Mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge aliyefariki Jumamaosi iliyopita, mdogo wake marehemu ambae amesema taratibu za kuupumzisha mwili wa marehemu zinaendelea katika makaburi ya familia huko Mkuyuni.

MAYWEATHERER NA MANNY WAWAGAWA WAMAREKANI

Floyd Mayweather VS Manny Pacquiao.. Kura ya Muhammad Ali iko upande huu !

Floyd Pac
50 Cent, Justin Bieber, Mike Tyson.. Hayo ni baadhi ya majina ya mastaa ambao walijitokeza kabisa na kusema kwamba wanaamini mkali wao Floyd Mayweather atamshinda Manny Pacquiao May 2 2015.
Mtoto wa Legend wa mchezo wa Ngumi DunianiMuhammad Ali ambaye anaitwa Rasheda Ali amesema kura ya baba yake iko upande wa Pacquiao; “My dad is Team Pacquiao all the way!”– Rasheda Ali.
.
Muhammad Ali akiwa na mwanae Rasheda.
Rasheda amesema baba yake huenda akawa mmoja ya mashabiki watakaojitokeza kushuhudia mpambano huo ambao kwa Muhammad ni kama utakuwa unamkumbusha enzi zake akiwa ulingoni.
Hutopitwa na habari yoyote inayonifikia na niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

ANA MIAKA 56 WATOTO 40

Mzee na watoto wake 40… kingine anachokiwaza ni hiki!!

babaUzazi wa mpango ni jambo ambalo husisitizwa mara nyingi  ili kuwa na familia bora na uwezo wa kutunza familia kutokana na idadi ya watoto wanaozaliwa.
Mike Holpin hakuona umuhimu wa ishu ya uzazi wa mpango,  mpaka sasa ana watoto 40 na bado anafikiria kuongeza wengine huku akiamini hata vitabu vya dini vinaruhusu hilo.
Mwanaume huyo mwenye miaka 56 mwenyeji wa Monmuothshire, Uingereza alipata mtoto wake wa kwanza akiwa na miaka 19 tu na kwa sasa mtoto wake wa kwanza ana miaka 37 huku wa mwisho akiwa na miaka mitatu.
mgongoWatoto hao amezaa na wanawake 20 tofauti na amesisitiza kuwa yupo tayari kuongeza wengine kwani hata vitabu vya dini vimeruhusu na ameamua kujichora tattoo zenye majina ya watoto wake mgongoni ili aweze kuwakumbuka.
Aliongeza kati ya wanawake 20 aliowazalisha sita ndio aliweza kuishi nao lakini baadae alitengana nao kutokana na tabia yake ya kutokuwa mwaminifu pamoja na kuwanyanyasa.
Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com