Kesi ya AT imeisha? Izzo B na show yake Mbeya na mazishi ya Abdul Bonge.
Ile kesi iliyokuwa imefunguliwa na mganga aliyedai kuwa anamdai msanii AT imemalizika rasmi jana baada ya kukata rufaa, AT
amesema kesi hiyo imemalizika rasmi jana baada ya mganga huyo kukata
rufaa lakini alikosa ushahidi na baadae iligundulika kuwa hakuwa na sifa
za kuwa mganga kwa kuwa alikuwa hajasajiliwa kufanya kazi za uganga.
Weekend hii msanii Izzo Bizness atafanya show Mkoani Mbeya ambayo imepewa jina la ‘Home Sweet Home Easter Season Concert‘, Izzo amesema show hiyo itafanyika tarehe 05 April, safari hii itakuwa tofauti kwa kuwa anategemea kuambatana na producer Duppy
kwa ajili ya kufanya usaili na mtu atakaeshinda atafanyanae kazi,
pamoja na surpise nyingi ikiwemo kuonyesha live video ya wimbo wake wa ‘Kidawa’ kwa mara ya kwanza.
Leo
wasanii mbalimbali pamoja na wadau wa muziki wamekutana Mkoani Morogoro
kwa ajili ya mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa kundi la Tip Top
Connection, Abdul Bonge aliyefariki Jumamaosi iliyopita, mdogo wake marehemu ambae amesema taratibu za kuupumzisha
mwili wa marehemu zinaendelea katika makaburi ya familia huko Mkuyuni.
No comments:
Post a Comment