Monday, March 23, 2015

MWANAMKE AFANYA KAZI YA KUOSHA MAITI KWA MIAKA MITATU KENYA

Kifahamu kilichomfanya mwanamke huyu kufanya kazi mochwari…

maiti kenyaKifo ni njia ya kila mmoja lakini watu wengi huogopa mtu aliekufa kutokana na hilo utakubaliana na mimi kuwa kunahitajika ujasiri wa aina yake kwa mtu kufanya kazi ambayo itamfanya kukutana na watu waliokufa kila siku.
Mwanamke mmoja nchini Kenya Magreth Wanjiru ambae ni mhudumu kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Nyeri ameonekana kuwa mwanamke mwenye ujasiri wa hali ya juu, kutokana na kufanyakazi ya kusafisha maiti na kuziweka dawa kazi ambayo anaifanya kwa muda wa miaka miwili.
Magreti amesema kuwa aliamua kujifunza kazi hiyo baada ya mama yake kufariki, ujasiri alioupata  kutokana na safari nyingi za kufika Hospitali  kumuona mama yake aliyeugua kwa muda mrefu na kumfanya asiwe na uwoga wa watu waliokufa.
Hata hivyo amepinga dhana kuwa mtu anaefanya kazi hiyo lazima awe anatumia kilevi au dawa za kulevya kazi inayoaminika kuwa inafanywa na wanaume pekee.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha .blogspot.com

No comments:

Post a Comment