Kingine usichokijua kuhusu maisha ya David Beckham…
Mara
nyingi mastaa mbalimbali wamekuwa wakiishi maisha ya kuwafanya
waonekana vyema mbele ya mashabiki wao na hata wengine kuishi maisha
ambayo si yao ili mradi wawe kivutio kwa mashabiki wao.
Hilo limekuwa tofauti kidogo kwa mkongwe wa soka duniani David Beckham ambaye pia ni mwanamitindo baada ya kusema amekuwa akimtegemea mke wake Victoria kwa asilimia tisini na tisa katika uvaaji wake.
Beckam ambaye ni baba wa watoto watatu
pia amesema yeye mara zote amekua akivutiwa na uhalisia wa maisha ya
watoto wake ambao wamekuwa wakimvutia kwa kiasi kikubwa.
Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid alisema
pia huwa anavutiwa sana na staili ya watoto wake kuanzia mavazi na
jinsi wanavyoishi,huku akimtolea mfano mtoto wake wa kwanza Brooklyn ambye amekiri kuwa amekuwa na mwonekano wa peke yake ambao humvutia wakati wote.
Mbali na Brooklyn amesema pia watoto wake wengine Romeo pamoja na Cruz nao wamekuwa wakimvutia wakati wote.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment