Monday, March 30, 2015

TUNASHANGAAA, VAN GAAL AIBUKA KIDEDEA

Van Gaal na tuzo maalum ya heshima kutoka Uholanzi.

vanManchester united ni kama haina bahati msimu huu kwani mpaka sasa bado haipo katika kiwango kizuri cha uchezaji na inakamata nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya England.
Pamoja na kutokuwa na kiwango kizuri lakini bosi wa klabu hiyo Louis Van Gaal ameweza kuibuka mshindi katika tuzo maarufu ya Anton Geesink ambayo hutolewa nchini Uholanzi.
Tuzo hiyo maalum hutolewa kwa mtu, mji au kundi la watu lililofanya vema katika michezo mbalimbali.
Van Gaal ambaye kikosi chake cha Man united hakiko katika kiwango kizuri msimu huu amepewa tuzo hiyo baada ya Uholanzi kuonyesha kiwango bora na kushika nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia nchini Brazil, mwaka jana.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment