Tuesday, March 24, 2015

CHAMA CHA SOKA ENGLAND YATAKA KUWABANA WANASOKA WA NJE

Kilichoamua Shirikisho la soka England kuhusu hatma ya wanasoka wa nje..

 MOJAAAShirikisho la soka nchini England FA limekusudia kuweka sheria itakayopunguza idadi ya wachezaji kutoka nje ya nchi za Umoja wa Ulaya watakaosajiliwa katika ligi kuu za nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa shirikisho hilo Greg Dyke amesema kwamba ligi kuu ya England ipo kwenye hatari ya kutowasaidia wachezaji raia wa Uingereza kama hatua za kupunguza wageni hazitachukuliwa mapema na sheria hiyo itaanza kutumika May 1 mwaka huu.
Katika mpango huo pia FA itaweka sheria ngumu kwa wachazaji wenye vipaji kutoka nchi nyingine waliokulia nchini humo.
Mikakati hiyo piaimelenga kuimarisha timu ya taifa ya England ambayo imekuwa haifanyi vizuri kwenye mechi za kimataifa ikiwemo kombe la dunia.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment