Abiria huyu aliandika barua kwa Rubani baada ya safari kuisha salama..
Ishu ya ajali ya ndege ya Germanwings ambayo ilipata ajali katika milima ya Alps
Ufaransa imekuwa ikizungumziwa sana hasa kutokana na ishu hiyo
kuonekana kwamba rubani mmoja aliebaki ndani ya chumba cha marubani
kuiangusha ndege hiyo kwa makusudi.
Watu wachache sana wanaweza kupakiwa
kwenye Bodaboda, Bajaj, au gari halafu akishuka anamshukuru dereva kwa
kumfikisha salama.. watu wengi hawana utamaduni huo wa kushukuru.
Nimekutana na hii barua ambayo imeandikwa na Bethanie ambaye alikuwa mmoja wa abiria aliyekuwa kwenye ndege, kamuandikia rubani Jai Dillon kumshukuru kwa kumfikisha salama.
Bethanie ameonesha pia kusikitishwa na tukio la ajali ya ndege ya Germanwings ambapo ndege hiyo ilikuwa na jumla ya watu 150.
No comments:
Post a Comment