Unaambiwa Oscar Pistorius amegeuka kuwa mwanasoka gerezani?
Oscar Pistorius
ameendelea kutumikia kifungo chake cha miaka mitano jela baada ya hivi
karibuni rufaa yake kukataliwa hivyo kufanya matumaini yake ya kuachiwa
kwa dhamana kupotea.
Mwanariadha huyo ambaye ni mlemavu
ameonekana akianza kuyazoea maisha ya gerezani ambapo hivi karibuni kuna
video ambayo inamuonesha akicheza mpira wa miguu na mwenzake wakiwa
ndani ya uwanja wa gereza alilofungwa mjini Pretoria Afrika Kusini.
Gereza la Kgosi Mampuru
ambapo mwanariadha huyo amefungwa liliweza kumpunguzia adhabu Oscar
huku akipewa uhuru wa kuongea na simu na hata kutembelewa na ndugu zake
jambo ambalo limeonyesha kumpa moyo.
Oscar alihukumiwa kifungo cha miaka
mitano baada ya kumuua mpenzi wakeReeva Steenkamp kwa kumpiga
risasiFebruary 14, 2013 nyumbani kwake.
https://www.youtube.com/watch?v=faWxQnLhqp4
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment