Tuesday, March 24, 2015

WEMA AIPA TANO MITANDAO YA KIJAMII

Kidoti na brand maalum,  Vee Money na Muigizaji Wema Sepetu na biashara za mitandaoni

IMG_1435Baada ya watu  kuhoji  ishu ya kampuni ya Kidoti kutengeneza ndala ambazo ni maalum kwa wanawake na kuonekama kama amewasahau wanaume,  Jokate ambae amesema kutakuwa na brand maalum ya wanaume na wataanza kuzipata muda wowote, akizungumzia kuhusu bei kuwa juu amesema watu wanaochukua ndio wanapandisha bei kutokana na gharama za kwenda kuchukua.
Screenshot-2014-06-20-at-00.00.45Mwanamziki  Vee Money wiki hii anategemea kuachia ngoma mpya aliyomshirikisha Rapa kutoka Afrika Kusini KO, akizungumzia ngoma hiyo amesema ni wimbo unayohusu mapenzi ya dhati ambao ni maalum kwa watu wote wanaopendana, kuhusu kumshirikisha KO amesema alikuwa anatamani kufanyanae kazi kwa muda mrefu lakini hakuwa na uhakika kama atapata ushirikiano lakini aliweza kuzungumza nae na kufanikiwa kufanya nae kazi.
wema_sepetuMuigizaji Wema Sepetu amesema mitandao ya kijamii inanafasi kubwa katika maisha yake hasa katika maswala ya utangazaji na kutolea mfano mtandao wa Istagaram na kusema, umerahisisha kazi kutokana na kutumiwa sana katika matangazo, yeye ameweza kujua maduka mengi na vitu vingi kupitia mtandao huo na endapo mtu akitaka apost kazi yake kwenye page yake ni kama dola elfu moja au elfu mbili lakini inategemea na makubaliano.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment