Baba wa Yemi Alade alifariki January 16, 2015, sasa wanapanga kufanya mazishi yake!!
Hapa
TZ tumezoea kuona mara nyingi ikitokea kuna msiba wa mtu yeyote huwa
haichukui muda mrefu kufanya mazishi, labda kuwe na sababu yoyote
itakayofanya mazishi yachelewe.. Nigeria iko tofauti, tulianza kuona
msiba wa mama yao jamaa wa P Square ambaye alifariki May 11 2012 na kuzikwa August 2 2012, baba yao Moses Okoye alifariki November 24 2014 na kuzikwa January 30 2015.
Huenda ulipata maswali kwamba kwanini mazishi ya wazazi wa mastaa hao yalicheleweshwa?
J.A. Alade ni baba wa msanii Yemi Alade
toka Nigeria, mzee huyo alifariki January 16 2015 na taarifa
iliyotolewa ni kwamba mazishi ya mzee huyo yatafayika May 7 mwaka huu.
Yemi Alade
alisema baada ya kumaliza ziara zake Ulaya atarudi na kuanza maandalizi
ya kumzika baba yake lakini hakuweza kueleza ni wapi mazishi hayo
yatafanyika.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment