Matokeo rasmi ya Uchaguzi Mkuu Nigeria yanaonesha Wanigeria wameamua hivi..
Siku ya MARCH 28 2015 itakuwa kwenye
historia za matukio ya kukumbukwa zaidi Nigeria, walikuwa wakifanya
Uchaguzi Mkuu ambapo macho ya wengi Afrika yalikuwa kwenye uchaguzi
huo.. Ushindani ulikuwa mkubwa kati ya Rais Goodluck Jonathan ambaye alikuwa madarakani na Muhammadu Buhari.
Kiongozi wa wa chama cha upinzani cha Nigeria ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Muhammadu Buhari amemshinda Goodluck Jonathan kwa zaidi ya kura Mil.2.5.
Goodluck Jonathan alimpigia simu Jenerali Buhari kumpongeza kwa ushindi huo wa kihistoria, ambapo Buhari anakuwa Rais wa kwanza kuongoza nchi hiyo akishinda kutoka Chama cha upinzani.
Nigeria ni moja ya nchi za Afrika ambazo
ziliwahi kukumbwa na misukosuko ya Mapinduzi ya Kijeshi, Jonathan
amesema katimiza ahadi yake kwamba Uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki;
“I promised the country free and fair elections. I have kept my word“– Rais Goodluck Jonathan.
Buhari ni mmoja ya wanasiasa ambao waliungwa mkono na mastaa wakubwa wa muziki Nigeria, Tiwa Savage na kundi la Mavins ni sehemu ya waliomsapoti.
No comments:
Post a Comment