Messi kaongezewa pesa Barcelona, unadhani anamzidi Ronaldo kwa sasa?
Haya
ndio majina makubwa zaidi kwenye soka kwa sasa.. Ushindani ni mkubwa
huku wengine wakivutana kuufikia muafaka, eti nani mkali kuliko
mwenzake, Ronaldo au Messi?
Mkongwe wa soka duniani Pele alinukuliwa na vyombo vya habari kwamba kura ya nani bora kati ya mastaa hao, yeye angempa Messi!
Leo ishu sio ukali wao uwanjani, ripoti ya mwisho kutolewa na goal.com ilionesha kuwa Ronaldo anaingiza pesa nyingi zaidi kuliko Messi.. Ronaldo anaingia
kwenye headlines za kukaa kwenye rekodi kubwa mbili alizoshikilia kwa
muda mrefu, ikiwemo hiyo na rekodi ya uchezaji bora wa soka duniani.
Lakini unaambiwa kwa sasa mpinzani wake mkubwa Lionel Messi amemzidi na kutajwa kuwa ndiye mwanasoka anaelipwa pesa nyingi zaidi na Klabu yake ya Barcelona katika list ya wachezaji wa soka, Messi analipwa paundi
milioni 26 zinatokana na mshahara huku nyingine zikitokana na dili za
mikataba aliyoingia na makampuni mbalimbali.
Kwa sasa Messi anaingiza jumla ya pound milioni 47.8 (zaidi ya Bil. 129) ambapo anamzidi Ronaldo ambaye anapokea pound milioni 39.7 (zaidi ya Bil. 106 Tshs) kwa wiki.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment