Msichana afia kwa mpenzi wake kilichofuatia ni hiki…
Tukio
moja lilimeibua hisia kubwa kwa wakazi wa kijiji cha Isyongo kaunti ya
nyamira nchini Kenya, baada ya Polisi kufukua maiti ya msichana mmoja Feidhi Omega 21, iliyokuwa imezikwa chini ya uvungu wa kitanda.
Taarifa zinasema kuwa binti huyo
alimtembelea mpenzi wake wiki mbili zilizopita lakini hakurudi nyumbani
kwao ndipo mama yake alipoanza kumtafuta na kuelekezwa kwa mpenzi wake Daniel Nyabuti,
huku akiwa na matumaini ya kumkuta mtoto wake akiwa hai, walipofika
nyumbani kwa kijana huyo Polisi walianza kumtafuta na kukuta kaburi
chini ya uvungu wa kitanda kwa kijana huyo ambako binti huyo alikuwa
amezikwa.
“Nikasilia
slipaz zimepatikana kwa njia ya huyo kijana baada ya hapo kufika tarehe
karibu tano hivi mwezi wa tatu nikachukua wazee wa nyumbani kuja hapa
tulikuwa watatu tukakuja mpaka nyumbani kwa kijana kuuliza huyo mtoto” Moraa mama wa marehemu
Hata hivyo haikuweza kujulikana kilichotokea na kusababisha kifo cha
binti huyo ingawa majirani wamesema walisikia akipiga kelele mtuhumiwa
huyo amekamatwa ili kujua chanzo cha kifo hicho.Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment