Wednesday, March 25, 2015

JAMANI----NI THIERRY HENRY HUYO

Cheki surprise ya Thierry Henry kwa hawa wanafunzi mtu wangu..

henryMkongwe wa soka wa zamani wa klabu ya Arsenal Thierry Henry aligeuka kichekesho baada ya kuwasuprise wanafunzi wa shule ya Pen-Y-Dre ya nchini Wales.
Henry aliingia darasa la wanafunzi hao na kuzuga kama mwalimu ambapo aliingia na kujitambulisha kisha kumpa tuzo mwanafunzi Emma Morgan ambaye ni mdogo kiumri aliyeshinda tuzo ya kuogelea huku akiwa amevalia wigi na miwani.
henr2
Haikuwa rahisi wanafunzi hao kufahamu kama ni yeye kutokana na wigi la kike alilokuwa amevaa pamoja na miwani vitu ambayo viliwachanganya na kushindwa kumwelewa.
henr3
Henry kwa sasa ni mtangazaji katika kituo cha Televisheni cha Sky Sports News akiwa kama mchambuzi wa soka kipindi ambacho hurushwa jumapili na alikwenda shuleni hapo kwa ajili ya ya kutoa tuzo hiyo.
henry4Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment