Ilivyokuwa pale Nou Camp jana.. Real Madrid VS Barcelona
Mechi huwa na fleva ya aina yake wanapokutana Barcelona na Real Madrid, majina ya mastaa waliopo kwenye timu zote mbili huwa ni kivutio tosha kufanya mashabiki wa mpira kuufurahia mchezo.. Cristiano Ronaldo VS Lionel Messi.
Jana March 22 2015 ilikuwa ngoma nzito kati ya Real Madrid na Barcelona.. Real ikiwa na list ya nyota wake C. Ronaldo, Benzema, huku Barca nao wakipanga safu poa iliyokuwa ikiongozwa na Messi, Suarez na Neymar.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinakamilika Barcelona walihakikisha hawautumii vibaya uwanja wao wa nyumbani Nou Camp ambapo waliibuka kifua mbele na kuwashinda Real goli 2-1.
Kwa matokeo hayo msimamo wa La Liga unaonesha Barcelona wanaendelea kuongoza ligi hiyo kwa jumla ya point 68 huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Real Madrid.
No comments:
Post a Comment