Sunday, March 29, 2015

KUTOKA MSIBANI KWA ABDUL BONGE



Abdu Bonge alifariki juzi Nyumbani kwake majira ya Jioni alipokuwa akiamulia ugomvi wa watu wake wa karibu ndipo alianguka vibaya kwenye sakafu na kupoteza fahamu kisha kufariki, Mwili bado uko hospitali kwa uchunguzi zaidi na taratibu zikikamilika leo March 30 mwili utasafirishwa kuelekea Morogoro Mbuyuni Kilometa takribani 100 kutokea Morogoro Mjini ambako ni Nyumbani kwa Marehemu. kwa sasa msiba upo Magomeni Njiapanda ya Kagera maskani ya Tiptop Connection

MB Doggy Msanii kutoka TipTop Connection akizungumza jambo na Rafiki waliotembelea Msibani hapo.

Mkubwa Fella akipitisha Daftari la michango kwa Ndugu na Jamaa waliofika Msibani.

No comments:

Post a Comment