Huwa unadata na nyumba nzuri nzuri? leo nimedata na hizi.
Furaha
nyingine kubwa kwa watu mbalimbali nikiwemo mimi ni kuishi au kukaa
kwenye sehemu ambayo moyo wangu umeridhia, yani kuanzia mazingira
yanayozunguka hapo ndio maana kwenye ndoto zangu za ujenzi siwezi kuacha
kupitapita nione idea ipi itanivutia.
Ujenzi wa nyumba nzima kama hizi unaweza
kuwa kikwazo kwako sababu ya kipato lakini mimi na wewe tunaweza kupata
idea hata chache za kuhamishia kwenye nyumba za uwezo wetu na bado
tukawa washindi.
Kwenye
hii nyumba ya kwanza nimevutiwa na jinsi walivyoweza kucheza na ukuta
mweupe kwa kuweka vitu ukutani na ndio ukavutia zaidi.
Hii nyumba ya pili ni kwa wale watu wangu wanaopenda kuwa na nafasi kubwa nyumbani.
Umependa nini ulichokiona kwenye hizi za leo mtu wangu?
No comments:
Post a Comment