Taarifa nyingine kubwa ni hii ajali ya ndege iliyotokea Ufaransa…
Matukio
makubwa ya ajali za ndege ambayo yametokea hivi karibuni na kuingia
kwenye headlines ni pamoja na ile ya Malasia Airlines iliyotokea mwaka
2014 ambayo ilipotea na mpaka sasa haijapatikana,na ajali nyingine ni ya
Trans Asia ambayo ilipata ajali kutokana na hali mbaya ya hewa na kuua
watu wote
Kuna
hii nyingine iliyotokea saa chache zilizopita imeripotiwa kuwa ndege ya
abiria inayomilikiwa na shirika la ndege la Germanwing Airbus A320
imeanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa.
Ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 142 na wahudumu 6 wa ndege walikuwa wakitokea katika mji wa Barcelona Uhispania kuelekea Duesseldorf, Ujerumani
Rais wa Ufaransa Francois Hollande
amesema kutokana na ajali ya ndege hiyo ambayo mpaka sasa bado
inaendelea kuchunguzwa kuna uwezekano mkubwa hakuna mtu yoyote anayeweza
kupona.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment