Ishu ya kupigana mabusu kwenye Headlines India!
Oktoba
mwaka jana chuo kikuu cha Zimbabwe kilipitisha sheria kupiga marufuku
wanafunzi wa kike na wa kiume kutopigana mabusu katika mazingira ya
chuo, kingine kilichozuiwa ni kukumbatiana na pia ishu ya wanafunzi wa
kike au wa kiume kuingia kwenye Hostel za wanafunzi wengine wa jinsia
tofauti na zao.
Safari
hii kuna taarifa ambayo imeingia kwenye headlines India baada ya
kupitishwa Sheria iliyowekwa na moja ya kijiji katika jimbo la Kusini
Magharibi ya kupiga marufuku kupigana mabusu hadharani na tabia nyingine
ambazo ni kinyume na maadili.
Uongozi wa kijiji hicho cha Salvador -de Mundo kilichopo Kaskazini mwa mji wa Panaji jimbo la Goa, imepitisha sheria hiyo huku ikiwaonya watu wanaotembelea eneo hilo dhidi ya vitendo kama hivyo.
Mmoja wa viongozi wa kijiji hicho Reena Fernandes alisema wameidhinisha sheria hiyo kutokana na malalamiko kutoka kwa wakazi kuhusu wapenzi wanaopigana busu hadharani.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment