Ishu ya Ufisadi kwenye Headlines KENYA.. Kingine alichokisema Rais Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta jana
amehutubia kikao cha Bunge la taifa hilo kilichofanyika March
26, amewataka maofisa wote wa Serikali waliotajwa katika ripoti
iliyotolewa waondoke ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.
”Serikali
yangu haina budi kuchukua hatua mahsusi ambayo inalenga kukomesha hili
zimwi la ufisadi mara moja, ufisadi umevuka mipaka na lazima nasi
tujifunge kibwebwe na kukabiliana nao, natarajia kuwa wale waliotajwa
katika ripoti hii watang’atuka mamlakani hadi pale uchunguzi
utakapokamilishwa.” Rais Kenyatta.
Ripoti hiyo iliyotayarishwa na tume ya
kupambana na ufisadi KACC imetoka wakati ambao kumekuwa na matukio mengi
ya ufisadi haswa kwa upande wa Serikali, Mawaziri 5, makatibu 6 na
Magavana 10, wametajwa kuwa miongoni mwa maafisa 175 wa umma
wanaolazimika kujiuzulu, huku kiongozi wa mashtaka ya umma ametakiwa
kuanzisha uchunguzi ndani ya siku 60.
Katika hotuba hiyo Kenyatta aliwaomba radhi Wakenya waliohujumiwa na Serikali hiyo katika uongozi uliotangulia.
”Ili
Wakenya waweze kusonga mbele na kusahau yaliyopita kufuatia hatua
zilizochukuliwa na Serikali zilizotangulia ni wajibu wangu kuchukua
fursa hii na kuwaomba msamaha wote waliodhulumiwa kwa njia moja au
nyengine, lazima serikali iombe radhi kwani fedha haziwezi kufuta
machungu ya mateso ambayo Wakenya wamepitia’‘–Rais Kenyatta.
Watu 1200 waliuawa katika ghasia hizo huku 650,000 wakiachwa bila makazi kutokana na vita baada ya uchaguzi wa mwaka 2008.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment