Baadhi ya jamii za watu waliofariki ndani ya msikiti baada ya milipuko Yemen
Zaidi ya watu 126 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa, baada ya watu wa kujitolea muhanga kujilipua misikitini nchini Yemen.
Watu hao wameuwawa katika milipuko iliyolenga misikiti katika mji mkuu Sanaa wakati wa sala ya Ijumaa.
Milipuko Yemen
Waandishi
Habari wanasema kuwa, misikiti yote miwili ni maeneo ya maombi kwa
waislamu wengi ambao ni Shia, maarufu kwa jina Houthis,
wanaodhibiti mji mkuu wa Sanaa.
Kwa miezi
kadhaa sasa, kumeshuhudiwa taharuki kubwa kati ya makundi hasimu nchini
Yemen, pamoja na makundi yaliyo na uaminifu na mtandao wa Al-Qaeda
yaliyo katika maeneo ya kusini na mashariki mwa taifa hilo.BBC
No comments:
Post a Comment