Mwanamke huyu akamatwa kwa ishu ya dawa za kulevya.. Njia aliyotumia kusafirisha ni story
Kila siku wauzaji wa dawa za kulevya
wamekuwa wakibuni njia mpya ya kusafirisha dawa hizo kwa nchi ambazo
zimepiga marufuku usafirishaji na utumiaji wa dawa hizo.
Mwanamke mmoja Uingereza amekamatwa baada ya kukutwa akiwa amebeba dawa za kulevya aina ya Cocaine ndani ya sidiria.
Mwanamke huyo Nola Williams alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Gatwick, akitokea Jamaica akiwa na mtoto mdogo pamoja na kijana anaejihusisha na biashara hiyo ambaye jina lake ni Raymond Goodison, ambao walikamatwa walipotaka kupanda treni kutoka uwanja wa ndege wa Gatwick kuelekea Victoria ndani ya London.
Wakati Polisi wakifanya ukaguzi
waligundua kilo moja ya cocaine yenye thamani ya dola £180,000 zikiwa
imeshonewa kwenye sidiria ya mwanamke huyo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment