Baada ya Rubani kuhusishwa na ajali ya ndege ya Germanywings kwa sasa wanaamua utaratibu mpya
Taarifa nyingine kuhusu ndege ya kampuni ya Germanywings
ilioanguka katika Milima ya Alps Ufaransa siku ya Jumanne March 24
zinasema kulingana na uchunguzi uliofanywa kwenye kisanduku cha kunasa
sauti katika ndege hiyo inaonesha rubani mmoja aliyekuwa ndani ya chumba
cha kuendesha ndege amehusika kusababisha ajali hiyo.
Uchunguzi
wao unaonesha rubani huyo alimfungia rubani mwenzake nje ya chumba cha
marubani na kuipeleka kwa kasi ndege hiyo eneo lenye milima hiyo na
kuigongesha huku abiria wakisikika wakipiga kelele kabla ya ndege hiyo
kuanguka.
Ndege hiyo aina ya Airbus 320 ilikuwa ikitoka Barcelona kuelekea Düsseldorf Ujerumani,
iligonga Mlima na kuwaua abiria wote 144, pamoja na wafanyakazi sita wa
ndege hiyo, maafisa usalama wa Ufaransa wanasema rubani Andreas alikuwa hai mpaka hatua ya mwisho ndege hiyo ikipata ajali.
Bado hawana uhakika kusema chanzo hasa
cha ajali japo Serikali ya nchi hiyo imekataa kuthibitisha kwamba tuio
hilo lina uhusiano na masuala ya kigaidi.
Kinachoangaliwa kwa sasa ni jinsi ya
kuweka utaratibu mpya wa kuwepo Sheria itakayowafanya Marubani wote
wawili kuwepo ndani ya chumba cha marubani wakati wote ndege ikiwa
safarini.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment