Umeskia hii ya mama kujifungua mara mbili ndani ya mwaka mmoja?
Tuliwahi
kuandika hapahapa www.tangakumekucha.blogspot.com stori ya mwanamke kujifungua watoto mapacha ambao walipishana
miezi miwili waliozaliwa katika moja ya hospitali huko Romania na
kuonekana kugusa hisia za watu wengi.
Hii
tena imetokea huko Uingereza baada ya mama mmoja kupata watoto wanne
ikiwa ni matokeo ya kushika ujauzito mara mbili ndani ya mwaka mmoja.
Sarah Ward mwenye umri wa miaka 29 alipata mapacha watatu ikiwa ni mwezi mmoja tangu ajifungue mtoto wake wa kwanza wa kiume,
Mwanamke huyo alijifungua mapacha hao
watatu ambao walizaliwa kabla ya muda huku mtoto wake wa kwanza akiwa
tayari na miezi nane.
Sarah amesema anashukuru kupata watoto
hao na amekua akitumia nepi zaidi ya 30 kwa siku kwa ajili ya
kuwabadilisha watoto wake lakini haoni kama ni gharama kutokana na
furaha aliyonayo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment