Tuesday, March 31, 2015

MAITI YAPATA AJALI WAKATI IKIPELEKWA KUZIKWA

Hii imeshtua wengi.. Mwili wa marehemu umepata ajali wakati wakienda mazishini

RIPHii story iko kwenye Headlines Indonesia.. Ilikuwa ni msiba wa mtu mmoja ambapo wakiwa njiani kwenda kwenye mazishi likatokea tukio jingine, story ikawa kubwa zaidi.
Waombolezaji walikuwa  wamebeba mwili wa marehemu kwenda makaburini kwa ajili ya mazishi, mwili wa marehemu uliokuwa umebebwa ulidondoka bila wao kujua na kuendelea na safari.. watu waliokuwa nyuma yao wakaona mwili huo katikati ya barabara.
Ilibidi wawaite na kuwaambia kwamba mwili wa marehemu walikuwa wameuacha nyuma yao, wakarudi kuuchukua na kuurudishia ndani ya jeneza na kuendelea na safari ya kwenda kuzika.
Video ya tukio hilo iliyowekwa katika mtandao imeshaangaliwa na watu zaidi ya 110,000 ndani ya siku mbili.


Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

1 comment:

  1. MAITI YAPATA AJALI WAKATI IKIPELEKWA KUZIKWA "Na Marehemu akafariki tena".

    ReplyDelete