Obama kaamua kutimiza ahadi ya kutembelea kwao KENYA?
Kila mtu anafahamu kwamba marehemu baba mzazi wa Rais wa Marekani Barrack Obama
ana asili ya Kenya, lakini mara nyingi amekuwa akiulizwa kwamba kwa
nini tangu amekuwa Rais wa Marekani hajawahi kutembelea kwenye nchi
hiyo.
Hilo swali kawahi kuulizwa zaidi ya mara
mbili, lakini alipokuwa South Africa mwaka 2013 alijibu kwamba kwa
sababu hajamaliza uongozi wake, basi tusubiri hiyo safari ya kutembelea
Kenya huenda ikawepo wakati wowote.
Taarifa kutoka Ikulu ya Marekani jana imetangaza kuwa Rais Obama atarajiwa
kwenda Kenya mwezi July 2015 ambapo atakuwa akihudhuria Mkutano mkubwa
wa kibiashara na ujasiriamali utakaofanyika Nairobi.
Labda kitu ambacho Wakenya wengi
hawakukipenda ni ishu ya Rais huyo kutembelea nchi nyingine kama
Tanzania, Senegal na Afrika Kusini lakini hakufika nyumbani kwao.
Mara ya mwisho Obama kufika Kenya ilikuwa mwaka 2006 ambapo wakati huo alikuwa bado Seneta wa Illinois, Marekani.
Ikulu ya Marekani wamesema wataendelea kutoa taarifa zaidi kuhusu safari hiyo.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment