Baada ya ugomvi wa Madirector wawili wa Tanzania, haya manne ni kutoka kwa Adam Juma.
Anayo
heshima yake kama Director wa video mkongwe kwenye kizazi cha
Bongofleva ambae baada ya kuona maneno yakiendelea kurushwa kati ya
Madirector wawili kwenye kizazi hikohiko, yani Nisher na Hanscana, Adam
ameamua kutoa maneno yake kama kaka.
katika sanaa za kijinga sana, hazileti maendeleo bali
chuki tu, vita kati ya madirector sio jambo la kushangilia hata kidogo,
kwani mtu ukiwa wa kwanza wa pili maana yake nini?
‘Mnapoteza
urafiki kwa umaarufu wa siku mbili, kitu hiki kilifanyika kwa Pfunk na
Mj, then dunga na mapigo then lamar, wako wapi hawa watu ambao ndio
mngongo wa mziki, ukiwaangalia hawa maproducer wote ni wakali ila ujinga
ndio umesabisha ubishani usiokua na maendeleo’
Kwenye sentensi ya tatu akaandika >>>
‘Tujifunze kupenda na kuangalia style za wenzetu sio kwa lengo la
kusema nani ni mkali au nani ni wa kwanza, kwa nia hiyo tutakuza sanaa,
sijawahi hata siku moja kufikiria kwamba nimfunike mtu flani au niwe on
top, bali nafanya kwa kadri ya uwezo wangu kuwa tofauti, mengine
nawaachia watazamaji’
‘Sitaki
kufananishwa na mtu yoyote yule kwa uzuri wala ubaya, kama hujaelewa
nachokifanya nunua camera fanya wewe, nawaonya nyie mnaogombana mkiwa
mmesahau mlipotoka, UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU. Hakuna aliyebora
kati yetu wote tunaudhaifu wetu’
No comments:
Post a Comment