Pale ambapo message inafanya afumaniwe na mke wa mtu
Story iliyosikika leo
inahusu ishu iliyotokea maeneo ya Mabibo Hostel ambayo inahusu kijana
ambae ni mwanafunzi wa chuo ambaye kulikuwa na taarifa kwamba ana
uhusiano wa kimapenzi na mke wa mtu.
Baada ya kukamatwa na mume wa mwanamke
huyo, mwanafunzi huyo amesema kuwa mume wa mwanamke huyo alimkuta akiwa
ndani kwake akijaribu kumshawishi mwanamke ili alale nae, lakini
anajitetea kwamba ni bahati mbaya tu imetokea hivyo.
Akizungumzia tukio hilo mume wa mke huyo
amesema alikuwa amelala akaona message inaingia kwenye simu ya mke
wake, alipomuuliza alimwambia hamjui mtu aliyetuma message hiyo..
mwanaume akamwambia amshawishi aje ili amuone.
Kijana huyo alipofika aliingia ndani na
kuanza kumbembeleza mwanamke huyo walale, mwanaume akajitokeza na kuanza
kumpiga.. mfukoni alikutwa na condom pamoja na shilingi 600.
Baadaye mwanaume huyo alimpeleka Polisi huku akiendelea kujitetea kwamba ni bahati mbaya imetokea hivyo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment