Kilichotokea chumba cha maiti wakati wa maandalizi ya mazishi..
Zimesikika story za watu kuzinduka
wakiwa mochwari.. Huyu kapata fahamu kwenye mazingira ambayo
yalisababisha mtu ambaye ana jukumu kufanya uangalizi wa maiti nae
kupata matatizo mengine.
Mwanamke mmoja Ujerumani alipata fahamu
akiwa ndani ya jeneza chumba cha kuhifadhia maiti, akaanza kujiburuza
kutoka ndani ya jeneza, jamaa ambaye anasimamia chumba hicho cha
kuhifadhi maiti akazimia baada ya kumuona.. alipozinduka mwanamke huyo
akamuuliza; “kwani hapa niko wapi?”, jamaa huyo akapiga simu kuomba msaada wa ambulance.
Ambulance ilifika na kumchukua mwanamke
huyo kumpeleka Hospitali ambapo siku ya pili yake akafariki tena wakati
akipata matibabu.
Polisi wanachunguza juu ya ishu ya
kilichofanya mwanamke huyo kuonekana amefariki kwa mara ya kwanza ambapo
ndugu wa marehemu huyo walimkuta akiwa hana fahamu kitandani kwake.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment