Kutokuelewana kwa Nahreel na Quick Rocka kumefikia hapa, walipokutana Club je?
Wote
tunapenda headlines nzuri kwenye bongofleva ndio maana inapotokea
kutokuelewana miongoni mwa watu wetu tunaowakubali zitafanywa jitihada
tu ilimradi tuyamalize kwa amani.Baada ya Mwandisji kuwakutanisha Matonya na Tunda Man na kuyamaliza, ilifanikiwa kubeba pande zote mbili za Nahreel na Quick Rocka ambao hawapatani.
Nahreel alikubali kuendelea kuusambaza upendo ambapo alianza kwa kusema >>> ‘Kiukweli nilikua sielewani na Quick na hii ni baada ya yeye kusema niliondoka kwenye studio yake Kiswahili yani bila kumuaga, huenda ni kweli niliondoka hivyo lakini Quick hakuniajiri mimi, nilikwenda kumsaidia kama msela wangu na kazi tulikua tunafanya kishkaji’
‘Nilikua
na mipango yangu ya kufungua studio na nikafungua lakini pengine labda
jamaa hakufurahia mimi kuondoka pale, natafuta jinsi ya kukaa nae na
kuongea kama binadamu ili tuweke haya mambo sawa, nina mpango wa kwenda
kuongea tuyamalize’ – Nahreel.Baada ya maneno ya Nahreel Quick akazungumza yafuatayo >>> ‘Hatukua na mkataba wa maandishi bali wa maneno ndio maana nikatangaza kwamba Nahreel sasa hivi yuko Switch, na alivyoondoka bila taarifa kibiashara na mimi ilinikasirisha, kama yuko tayari kuyamaliza mimi niko poa… kama anajua kweli alikosea na sasa anataka amani mimi sina tatizo’
No comments:
Post a Comment