Sunday, March 22, 2015

UDANGANYIFU WA MAJIBU YA KITIHANI INDIA NAO WAMO

Udanganyifu huu wa mitihani India nao kumbe wamo

India Cheating on ExamsTabia ya baadhi ya wanafunzi kupenda kuigilizia majibu wakati wa mitihani si jambo la ajabu lakini kwa kilichotokea nchini India kimeweza kuchukua headlines kwa kiasi kikubwa.
wizi
Udanganyifu wa mtihani umekuwa jambo la kawaida katika Jimbo la  Bihar na kuna picha mpya zimetolewa zikionyesha tukio hilo likifanywa kwa kiwango kikubwa.
Wazazi na marafiki wa wanafunzi hao walipigwa picha wakipanda ukuta wa vyumba vya kufanyia mitihani ili wawape majibu wanafunzi katika mitihani kwenye moja ya shule za upili nchini humo.
wizi2
Mpiga picha Dipankar ambaye alipiga picha hizo katika wilaya ya Saharsa amesema alipoingia katika chumba cha mtihani na kuchukuwa picha hizo wanafunzi hawakujali nakuendelea na kuigilizia majibu waliyopewa na ndugu zao.
Tayari baadhi ya wanafunzi waliohusika na udanganyifu huo wamefukuzwa shule huku wazazi wao wakifunguliwa mashtaka na bado uchunguzi unaendelea.
Mtihani huo ulioandaliwa na bodi ya shule ya Bihar (BSEB) ulianza Jumanne na unatarajiwa kuendelea hadi tarehe March 28.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment