Friday, March 27, 2015

WANANCHI WASUSIA MAITI NA KUIPELEKA KITUO CHA POLISI

Kisa cha Polisi kususiwa maiti safari hii ni Kenya mtu wangu..

SONY DSCKumekuwa na malalamiko mengi ya kwamba Polisi wanawaonea raia, siku chache zilizopita kulikuwa na story ya tukio la Polisi kususiwa maiti ya kijana mmoja hapa TZ ambapo watu waliosusia maiti hiyo walidai Polisi walihusika kusababisha kifo cha mtu huyo, safari hii imetokea Kenya.
Katika kaunti ya Nyeri nchini Kenya kuna tukio lililotokea juzi March 26 ambapo watu waliokuwa wakiomboleza walichukua mwili wa mtu mmoja na kwenda nao katika kituo cha Polisi cha Mkurueni  wakidai Polisi walihusika na kifo cha mtu huyo.
Waombolezaji hao walichukua mwili huo katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Nyeri na kuandamana hadi kituo hicho kwa madai mwanaume huyo alipigwa risasi na Polisi wa kituo hicho, walikutana na maafisa wa Polisi ambao walijaribu kuwazuia lakini waliwashinda nguvu na kuweka jeneza kwenye mlango wa kituo hicho na kuondoka.
Polisi waliwarushia mabomu ya machozi  ili kuwatawanya, baadaye walikubaliana hali ikakaa sawa ambapo ndugu wa marehemu huyo walikubali kuuchukua mwili na kwenda kufanya mazishi.

No comments:

Post a Comment