Utaratibu huu umerudiwa tena Sierra Leone katika mapambano na Ebola..
Sierra
Leone ni nchi ambayo imepata athari kubwa zaidi kutokana na ugonjwa wa
Ebola tangu ugonjwa huo ulipoanza zaidi ya mwaka mmoja sasa, athari yake
sio kwa watu waliofariki ama kupata maambukizi ya Ebola pekeyake,
imefikia hatua hata ya uchumi wa nchi hiyo kuwa kwenye hali mbaya, shule
zimefungwa na vitu vingine vingi kusimama.
Hii sio
mara ya kwanza Serikali kutoa agizo kama hili ambalo limetolewa la watu
wote kukaa ndani kwa siku tatu kuanzia leo March 27 mpaka Jumapili
March 29 ili wafanye ukaguzi wa nyumba hadi nyumba kujua kama kuna watu
ambao wana dalili za ugonjwa huo waweze kuwapata na kusaidia watu
wengine wasipate maambukizi hayo.
Siku ya
Ijumaa zimetolewa saa mbili tu kwa waislamu kwenda kuswali, siku ya
Jumapili pia zitatolewa saa tano kwa ajili wakristo kwenda kusali.
Mataifa matatu ya Afrika Magharibi
yalioathiriwa vibaya na Ebola ni Sierra Leone, Liberia pamoja na Guinea
na zimepanga kuhakikisha zinatokomeza ugonjwa huo ifikapo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment