Maamuzi ya binti huyu kwa mama yake nayo kwenye headlines!!
Matukio
ya wazazi kuwa na ugomvi na watoto wao wa kuwazaaa wenyewe huwa ni
jambo la kawaida kutokea ndani ya familia lakini inapofikia hatua ya
watu hao kutaka kutoana uhai kwa lengo la kulipiza kisasi huleta picha
nyingine kabisa kwenye jamii.
Hii imetokea huko Marekani baada ya mama
mmoja kunusurika kifo mara mbili baada ya mtoto wake kumwekea sumu ya
kuondoa madoa kwenye kinywaji chake kisa kikiwa ni baada ya
kumnyang’anya simu yake aina ya Iphone.
Mtoto huyu mwenye miaka 12 katika jimbo la Colorado Marekani amefunguliwa mashtaka ya kuua na amekiri kuwa alitaka kumuua mama yake ili kulipiza kisasi kwa sababu alichukua simu yake.
Mara ya kwanza mtoto huyo alimwekea mama
yake sumu aina ya Chlorine kwenye kinywaji na mama yake hakuweza
kubaini ingawa alisema alisikia harufu lakini alihisi glasi aliyotumia
haikuoshwa vizuri.
Mama yake aliwaambia maafisa wa polisi
kuwa alishangaa aliponusa harufu ya sabuni baada ya kunywa mchanganyiko
huo uliotayarishwa na mwanaye huyo.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment