Tulizipokea taarifa za kifo cha Abdul Bonge wa Tiptop Connection ila hiki ndio chanzo cha kifo
Saa
zinahesabika toka Tanzania na familia ya bongofleva ipokee taarifa za
msiba wa Abdul Bonge Mwanzilishi wa kundi maarufu la Bongofleva Tiptop
Connection lenye wanachama kama Tunda Man, Madee, Dogo Janja na wengine
waliopita kama Keisha, Cassim Mnganga na MB Dogg.
Jioni ya March 28 2015 ndio taarifa
zilianza kusambaa katika mitandao lakini chanzo cha kifo cha ghafla cha Abdul hakikuwa
kimesemwa lakini mdogo wake ambae ni Babu Tale amewka bayana.
na kusema >>> ‘Kuna mshkaji wetu mmoja alikua anagombana na
mke wake jirani yetu, wakamfata hapa Abdul aende… mara ya kwanza na ya
pili akakataa, mara ya tatu akasema ngoja aende’
‘Alivyoenda
ukapita ukimya kidogo, baadae kuna mtu akaja kumuita kaka yetu mkubwa
mwingine na kumwambia nenda kamsaidie kaka yako mkubwa amedondoka, kaka
yangu baadae akanipigia simu akasema Bonge kama amezimia lakini sidhani
kama atapona sababu wakati wa kuamulia ugomvi alianguka baada ya
kusukumwa nafikiria aliangukia kichogo, kumpeleka Hospitali Manzese
wakasema ameshafariki‘ – Babu Tale.
Hutopitwa na habari inayonifikia na niko tayari kukutumia muda wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment