Ajali ya ndege:rubani alifungiwa nje
Ndege ya Germanwings ilipokuwa ikisafiri katika anga la Duesseldorf nchini Germany mwaka 2014.
Mkurugenzi
wa shirika la ndege la Germanwings, Thomas Winkelmann amesema wasafiri
72 kati ya 144 walikuwa raia wa Ujerumani.
wengine
walikuwa ni kutoka nchi za Australia, Argentina, Iran, Venezuela,
Marekani, Uholanzi, Colombia, Mexico, Japan, Denmark na Israel.
Uchunguzi
wa awali wa sauti zilizokuwa ndani ya kifaa cha kurekodia sauti ya
ndege iliyoanguka Ufaransa unaonesha kuwa moja wa marubani wa ndege hiyo
alikuwa amefungiwa nje ya eneo la marubani wakati ndege hiyo
ilipoanguka.
Wanafunzi katika shule ya Haltern-am-See nchini Ujerumani wakilia baada ya wenzao kupata ajali kwenye ndege ya Germanwing.
No comments:
Post a Comment