Tuesday, March 24, 2015

MCHINA AWEKA SHERIA KALI KUINGIA MGAHAWANI MTU MWEUSI KENYA

Ikifika saa moja kama wewe ni mtu mweusi huruhusiwi kuingia Mgahawa huu Nairobi !!

19.si
Kumekuwa na story nyingi toka Kenya kuhusiana na matukio ya uvamizi na mauaji ambayo yanahusishwa na Kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab.. Watu wengi wanahofia usalama wao hasa maeneo ambayo yana mkusanyiko mkubwa wa watu.
Mgahawa mmoja unaomilikiwa na watu wenye asili ya China maeneo ya Kilimani, Nairobi Kenya umeingia kwenye Headlines kutokana na sheria waliyoweka ya kuwazuia wakenya na mtu yoyote ambaye ni mweusi kungia kwenye mgahawa huo baada ya saa 11 jioni.
Mgahawa huo umeweka sheria hiyo kali kutokana na tukio la uvamizi lililotokea mwaka jana, kwa madai kuwa genge la majambazi waliingia katika mgahawa huo wakijifanya kuwa ni wateja, baadaye wakawateka na kuwapora wateja pamoja na pesa zote za mauzo ya mgahawani hapo.
z137-500x250Afisa uhusiano katika mgahawa huo Esther Zhao amesema hawaoni kama kuna ubaya kuhusu kanuni hiyo waliyojiwekea japo wanaharakati wa Kenya wanadai imekaa kibaguzi kwa misingi ya rangi.. Iwapo kuna mtu yoyote mweusi akitaka kuingia baada ya saa 1 jioni atatakiwa aingie kwenye Mgahawa huo akiwa na mdhamini ambaye ni mzungu, mhindi au mchina.
Kwa upande wa Afisa wa masuala ya raia nchini humo, Otiende Amollo amesema sheria hiyo ni kinyume cha sheria, inakiuka uhuru wa wakenya na inawafanya watu weusi kuonekana kuwa ni majambazi na kuitaka tume ya kupigania haki za kibinadamu kuushtaki mgahawa huo kwa kukiuka maadili.
Msemaji wa Mgahawa huo amesema waafrika wachache wanaruhusiwa kwa sababu ni waaminifu na wateja wao wamefurahia sheria hiyo kali ambayo wanaona inawahakikishia usalama wao kwa sababu  ni vigumu kugundua watu wanaojihusisha na kundi la Al Shabaab iwapo wakiingia kama wateja.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment