Mzee na watoto wake 40… kingine anachokiwaza ni hiki!!
Uzazi
wa mpango ni jambo ambalo husisitizwa mara nyingi ili kuwa na familia
bora na uwezo wa kutunza familia kutokana na idadi ya watoto
wanaozaliwa.
Mike Holpin
hakuona umuhimu wa ishu ya uzazi wa mpango, mpaka sasa ana watoto 40
na bado anafikiria kuongeza wengine huku akiamini hata vitabu vya dini
vinaruhusu hilo.
Mwanaume huyo mwenye miaka 56 mwenyeji wa Monmuothshire, Uingereza alipata
mtoto wake wa kwanza akiwa na miaka 19 tu na kwa sasa mtoto wake wa
kwanza ana miaka 37 huku wa mwisho akiwa na miaka mitatu.
Watoto
hao amezaa na wanawake 20 tofauti na amesisitiza kuwa yupo tayari
kuongeza wengine kwani hata vitabu vya dini vimeruhusu na ameamua
kujichora tattoo zenye majina ya watoto wake mgongoni ili aweze
kuwakumbuka.
Aliongeza kati ya wanawake 20
aliowazalisha sita ndio aliweza kuishi nao lakini baadae alitengana nao
kutokana na tabia yake ya kutokuwa mwaminifu pamoja na kuwanyanyasa.
Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment