GWAJIMA AZIRAI AKIHOJIWA NA POLISI, NI KUFUATIA MANENO YA KASHFA DHIDI YA KADINALI PENGO
Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima, Josephat Gwajima, akiwa amelazwa hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam jana
Gwajima akizungumza na waandhishi wa habari alipowasili kituo kikuu
cha polisi cha kati jijini Dar es Salaam.
Gwajima, wakili wake, wafuasi na walinzi wake wakielekea kituo kikuu cha polisi kati.
Gwajima kabla ya kuzirai
Gwajima ambaye anaelezwa kumiliki helikopta na magari ya kifahari, aliingia matatani baada ya mkanda wa video uliomrekodi akihutubia mamia ya wafuasi wake kwenye viwanja vinavyotumiwa na kanisa lake, vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam wiki iliyopita alidaiwa kumkashifu kwa maneno makali, Askofu Mkuu wa jimbo Kuu la Dar es Salaam, kanisa Katoliki, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, kuwa hafai kuwa kiongozi wa kanisa.
Gwajima alimtuhumu kwa kile alichokiita “kuwasaliti viongozi wenzake wa kanisa waliokubaliana kuwahamasisha waumini wao kutoipigia kura katiba pendekezwa.
Hata hivyo Kadinali Pengo alipinga msimamo huo wa viongozi wenzake, na kuwataka waache kuwaamulia waumini na badala yake waumini wenyewe waachwe wajiamulie.
Hutopitwa na habari na niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment