Tuesday, March 17, 2015

FAINI YA SHILINGI 200 KSH, YAMUGHARIMU KUSOTA GEREZANI NA KUUGUZA MAJERAHA

Ishu ya mtuhumiwa kutoroka Mahakamani safari hii ni Kenya !!

DSC00660
Mwezi December 2014 kulikuwa na story ya mtuhumiwa mmoja kuuawa kwa kupigwa risasi wakati alipokuwa akijaribu kutoroka Mahakama ya Kisutu kwa kuruka ukuta wa Mahakama hiyo, story kutoka Kenya leo inafanana na hii.. inahusu mtuhumiwa mmoja kufanya jaribio la kutoroka kutoka Mahakama ya Machakos.
DSC00659
Mtuhumiwa huyo alijaribu kutoroka lakini askari wakampiga risasi mkononi na mguuni akiwa juu ya ukuta, majeraha hayo yalimfanya ashindwe kukimbia, akakamatwa.
DSC00661
DSC00664
Mahabusu huyo alifikishwa Mahakamani kwa kosa la kufanya vurugu baada ya kutolewa  hukumu yake ilikuwa alipe faini ya Kshs 200, jaribio lake la kutoroka limefanya awe na kesi nyingine mpya kutokana na kufanya kosa hilo.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia  www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment