Hadithi hii inaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Tiba Asilia kilichopo Chuda Tanga, Mkombozi Sanitarium Clinic. Mabingwa wa magonjwa sugu yakiwemo ya Kisukari, Figo, Saratani na mengi mengineyo. Wapo Chuda Tanga. simu 0654 361333
NILIJUA
NIMEUA (2)
Nikadhani
ataanza tena kulalamika kutaka kupunguziwe kiasi cha pesa. Lakini haikuwa
hivyo, alifungua mkoba wake akatoa noti ya shilingi elfu tano na kuniambia.
“Shika”
Niligeuka
nikaipokea kisha nikamfungulia mlango.
Akashuka
haraka na kukimbilia kwenye baraza ya ile nyumba. Wakati anabisha mlango
nikaiondoa teksi.
Nilirudi
katika egesho langu lililokuwa karibu na hospitali ya Ngamiani.
Nililipendelea
egesho hilo kwa maana. Kwanza lilikuwa karibu na hospitali ambapo mara kwa mara
kunakuwa na wagonjwa wanaohitaji huduma ya teksi. Pili nilikuwa peke yangu na
tatu kulikuwa na mahoteli mengi yaliyokuwa karibu na hapo na kufanya nipate
wateja wengi.
Wakati
naliegesha gari nilisikia mlio wa simu ndani ya gari. Nikashituka na
kudhani ilikuwa simu yangu. Lakini niligundua haikuwa simu yangu. Simu yangu
haikuwa na mlio kama huo niliousikia.
SASA ENDELEA
Nikatega
masikio yangu ili nijue mlio huo ulikuwa unatokea wapi. Nikapata jibu. Mlio huo
ulitoka nyuma yangu. Nikageuza kichwa na kutazama nyuma. Ndipo nilipoiona simu
ikiita kwenye siti.
Mara moja
niligundua kuwa yule msichana niliyempakia alisahau simu yake. Ilikuwa simu
ileile aliyokuwa akiitumia wakati nimempakia.
Sikuweza
kujua ni nani aliyekuwa anapiga. Iliwezekana alikuwa yeye mwenyewe,
aliamua kupiga baada ya kugundua kuwa aliisahahu simu ndani ya teksi yangu. Au
alikuwa ni mume wake ingawa sikuwa na hakika kama alikuwa na mume.
Nikajiuliza
niipokee ile simu au nisiipokee? Nikapata jibu kuwa nisiipokee kwa vile sikujua
nani anapiga na isitoshe haikuwa ikinihusu.
Baada ya
kuita kwa muda simu ikakatika lakini baadaye kidogo simu ikaita tena. Nikaiacha
iite.
Kwa vile
nyumba aliyoingia yule msichana ninaifahamu nitampelekea wakati wowote, nikajiambia.
Hata hivyo
sikupata amani kwani simu ilikuwa ikiita kwa mfululizo. Ufumbuzi ulikuwa
niizime au niipeleke kwa mwenyewe haraka. Kwa vile nilishindwa kuizima niliamua
niwashe teksi nimrudishie mwenyewe.
Mvua sasa
ilkuwa imeacha kabisa. Nilifika katika mtaa aliokuwa akiishi yule msichana.
Tangu natokea katika mtaa huo niliona msichana amesimama kwenye baraza ya ile
nyumba akiwa amejaa wasiwasi. Nilipokaribia zaidi niligundua kuwa alikuwa ni
yule msichana niliyempakia.
Niliposimamisha
teksi mbele ya ile nyumba aligutuka, akanikodolea macho ya tashiwishi.
Mara moja
akashuka kwenye baraza na kuja kwenye mlango wa teksi wa dereva.
“Kaka
umeniletea simu yangu?” akaniuliza kwa matumaini.
Kwa kutaka
kumshitua a mimi nikamuuliza.
“Simu gani?”
“Jamani
nilisahau simu yangu kwenye siti. Simu yenyewe niliinunua juzi tu shilingi laki
tatu”
Nilipoona
amehamanika nilimwambia.
“Hebu
angalia kwenye siti uliyokuwa umekaa”
Akasogea
mlango wa nyuma na kuchungulia kwenye dirisha.
“Si ile
pale!” akasema huku akifungua mlango.
Aliingia
ndani ya teksi akaichukua ile simu na kutoka.
“Asante
kaka. Kumbe ulikuwa unanitania!”
Sote
tukacheka. Huzuni ilikuwa imeshamtoka.
“Wewe ni
muaminifu sana. Nitakuwa nachukua teksi yako kila siku” akaniambia.
“Kwaheri,
nakwenda zangu” nikamuaga.
“Ulikuwa
umeniletea simu yangu. Asante sana kaka, endelea kuwa na moyo huo huo”
“Asante
bibie”
Wakati natia
gea niondoe gari sauti yake ikanisitisha.
“Nipe namba
yako. Nitakuhitaji tena siku nyingine”
Nikamtajia
namba yangu.
Je nini
kitaendelea? Usikose kuendelea na hadithi hii kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment